Kenya News in Swahili and English

Serikali Inawafahamu Wafuasi wa Mungiki.

Kuna wasiwasi unaoonekana kutanda katika mji wa Thika nchini Kenya, kuhusu kuendelea kwa shughuli za genge la wahuni la Mungiki katika maeneo ya Githunguri, Kiambu, na hata Muranga. Jambo ambalo linaoonekana kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa sheria katika biashara ya Matatu.  Kikundi hicho kinasadikika kueneza kurejewa kwa imani za jadi za kabila la kikuyu; lakini hata hivyo kimetuhumiwa kwa mauaji, unyang’anyaji na ulaghai.  

Wafuasi wa kikundi hicho wanafanya shughuli zao mbele ya macho ya Serikali ya Kenya. Kila Matatu  inalipa kiwango fulani cha pesa ili kuweza kuwasafirisha wateja toka sehemu moja hadi nyingine. Mbali na hayo, wanaitisha kiwango kikubwa cha pesa kila mwezi kwa ajili ya usalama. Genge hilo linafanya kazi ya kusafisha magari, na kudai kila mtu alipe ada ya matumizi ya barabara. Kiwango cha pesa wanachoitisha ni kikubwa sana na wengi hawawezi kulipa kutokana na umasikini walio nao. Hali hii imesababisha msuguano kati ya magenge na wafanyikazi wa Matatu. Serikali yetu inalifamu genge hili na ingekuwa vyema kama wangewasaidia wenye matatu kukomesha genge hilo mara moja.

Mwaka jana, genge hilo lilianza kudhibiti biashara yenye faida ya “chang’aa” (pombe) kwa madai kwamba watengenezaji walitakiwa kulipa ada ya shillingi 2000. Watengenezaji walipinga madai hayo na hapo genge hilo liliharibu biashara hiyo. Katika jitihada ya kutuliza hali, ufumbuzi wa matatizo ulitokea. Wengi waliohusishwa kwa matatizo hayo walidai kwamba kama serikali ingetimiza wajibu wake kwa kujenga makazi na huduma zingine za msingi kama maji na umeme, basi hawangetaabishwa na genge hilo. Umasikini umewalazimisha wakaaji wa vitongoji hivyo kufanya biashara ambazo serikali inadai siyo halali. Mwaka 2003, serikali ilitangaza kwamba ingejenga nyumba zaidi ya 150,000 kwa watu wa makazi duni. Miaka mitano baadaye, ahadi hii bado haijatekelezwa. Wakenya wenzangu, inapaswa kubadili mfumo mzima wa utawala, na jambo muhimu zaidi ni kuwa na sera ya kutoa mwongozo wa makazi na kutoa huduma katika maeneo ya makaazi duni.

Serikali ya Kibaki imeshindwa kuwasaidia wakaaji hawa katika kipindi hiki. Wakazi hawa wamechanganyikiwa akili na kushindwa kwa nini serikali haiwezi kuwapatia makazi au huduma. Wakaaji wa Kibera, Mathare na wenye matatu  yafaa wajitoe na uzoefu wao, hofu zao na matarajio na kuonyesha dunia vile wanavyokabiliana na hali kama hii isiokuwa ya kibinadamu. Mara nyingi watu ambao hawaishi katika makazi duni ndio ambao wanazungumzia masuala kuhusu makazi duni. Wakati huu, serikali ya Kibaki imewaangusha tena. Asilimia 60 ya wakaaji wote wa mji mkuu wa Kenya wanaishi katika makazi duni na hawawezi kuishi maisha ya heshima. Serikali imeshindwa! Kibaki asipewe kipindi kingine mbali Wakenya wamchague rais tofauti kuona kama watapata mabadiliko, kwani masilahi na usalama ya binadamu ni ya maana kuliko vitu vingine.

Hivi leo, genge hilo limevuruga wananchi na kuharibu biashara ya Wakenya. Ningeomba serikali irefushe mkono wake na kulichomoa genge hilo mara moja. Kila Mkenya anaelewa wanachama wa Mungiki wanakaa Mathare na vitongoji vidogo-vodogo hasa Nairobi. Serikali pia inafahamu vyema kabisa hili genge linausumbuvu sana kwa uchumi wa Kenya kwa jumla.

Munala Wa Munala

Advertisements

MarchUTCbThu, 29 Mar 2007 21:41:23 +0000000000pmThu, 29 Mar 2007 21:41:23 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: