Kenya News in Swahili and English

Mwenzako Akinyolewa, Chako Tia Maji

Inanikera sana kuona bado mpaka sasa kuna kile kinachoitwa watu weusi. Tumedharauliwa na Wazungu wengi wametuona kama watu wajinga kwa misingi mingi. Waafrika tunaishi kwenye pango na tunapotoka nje, tunarudishwa pangoni mara moja ili tusionyeshe aibu.Waswidi wengi hawajui chochote kuhusu mabadiliko ya kijamii hasa yale ya Afrika.Tunaendelea kuwa maskini na tunaendelea kuzaa umasikini kila siku. Je! Hali hii itaisha lini? 

Wengi mnaelewa ghasia na vurugu zilizotawala siku ya jumamosi mwendo wa 12 asubuhi. Kundi la walinzi lilibabaisha Bi Winne Mukaru na Bwana Okoth Osewe wa shirika la habari

la Kenya Stockholm Blog (KSB). Walidhulumiwa na hao walinzi kiwango ambacho siwezi nikaeleza kwa maneno. Baada ya kuona yale yaliyotokea hapo jumamosi, ningependelea kutizama hali hii kwa karibu. Stori hii inaanzisha chanzo cha kushindwa kuungana kwa Waafrika hasa Wakenya. Hapa jijini Stockholm kuna vituo vingi sana vya kudhulumu Waafrika, kama sio sahihi sana, msangi mdogo nisaidie. Kadri siku zinavyozidi, mateso yanaendelea kuonekana wazi. 

Nitazidi kukataa na kushawishika kuwa Afrika itaendelea. Nilipozaliwa, sikujua ni wapi naelekea na ni wapi natoka. Niliona dunia nzuri sana maana niliona dunia isiyokuwa na majukumu. Badala yake, mimi nilikuwa naidai dunia. Ni lazima tule, tusome, tuvae, tutibiwe na hata tupendwe na watu. Leo hii, naona dunia imebadilika. Wengi wa watu ni mafukara wakubwa, maskini, majambazi na matapeli na hata wahuni. Hali hii ngumu imeletwa na nani? Wengi wanalala kwenye vipembezoni vya maduka, kwani kwao usiku na mchana haina tofauti. Serikali yetu ya Kenya imekataa katakata kuwalinda wakenya hata hapa ng’ambo. 

Sehemu nyingi wanazokaa Waafrika hazina huduma kama zile zinazokaliwa na Waswidi. Waafrika tunapewa kazi duni na chafu ukilinganisha na wenyeji. Mkate, mayai, nyama, mchele, soda na hata hospitali za bure zipo. Je! mbona tunaendelea kuwa masikini na hali yetu haibadiliki? Hatuweki akiba na maisha ndiyo hayo. Dhahabu ya Afrika inapendeza hapa ulaya lakini watu wa Afrika hawapendezi. Wanyama Afrika ni wazuri na wanafurahisha kuliko Waafrika. Mbwa na paka zina sifa nzuri kuliko Mwaafrika. Bara
la Afrika lilipamba ulaya lakini kuingia ulaya ni vikwazo. Lazima Waafrika tuwe imara na kutuetea haki zetu hapa.
 

Siku zote Wazungu hutafuta misamiati ya kupambaza Waafrika kwa ukorofi . Wametuibia utajiri wetu na hatuwezi kukubali kuibiwa haki zetu pia. Mali ya dunia ni ya wote kama vile demokrasia ni ya wote. Uchumi uliojenga Ulaya ulitoka Afrika, lakini sisi sasa wenye uchumi huo hatuwezi kuutumia kubadilisha maisha na mastakabali yetu. Lazima tujiamini ili kusonga mbele kwa mbwembwe kama Wazungu walivyo. Natamani na nazidi kutamani kuwa wakaazi wa Sweden ni sawa, na mali yao ni ya wote, na wote wana dhamana ya kuitumia kwa manufaa ya umma. Sisi ni kundi moja, japo wengine ni warefu, wafupi, wanene, wembamba na hata wengine ni rangi tofauti. Kwa Bi.Winnie na Bw.Osewe msife moyo, mapambano yataendelea na haki itatekelezwa kona zote za dunia.  

Munala Wa Munala

Advertisements

MarchUTCbTue, 20 Mar 2007 00:13:28 +0000000000amTue, 20 Mar 2007 00:13:28 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: