Kenya News in Swahili and English

“Mwacha Mila Ni Mtumwa.” Asema Bw. Kaggiri.

Bwana Alex Wagunya Kaggiri amekaririwa leo hii akisema kwamba ni dhahiri kuwa, ni ndoto ya mchana na katu lugha ya kimombo haiwezi kuwakomboa Wakenya kutoka kwenye minyororo ya wakoloni. “Wakenya lazima watunze lugha yao ya mama au Kiswahili.” 

Bw. Kaggiri ambaye pia ni mwalimu wa hesabu, aliendelea kusema kwamba, Wakenya hasa wale walio hapa Skandinavia, wanagawanyika kwa sababu ya mambo madogo madogo, na ingekuwa vyema sana kama wangeungana na kuindeleza lugha ya taifa ambayo ni Kiswahili. Alisifu kundi la blogi ya Jamii kwa kuanzisha mradi wa kuandika habari kwa lugha ya Kiswahili. Kwa maoni yake, lugha ya kimombo ni lugha ya unyanyasaji, wasaliti, mabepari na kasumba zao. 

Inastajaabisha sana kuona Wakenya tumebaki nyuma sana kwa mambo ya lugha zetu za nyumbani. Badala yake, tumeigeuka nchi yetu na kukataa lugha ya taifa letu. Ni jambo la busara sana kuona watoto wetu wanaweza kuongea lugha ya Kiswahili. Hawa ndio viongozi wa kesho na wasipoweza kuongea lugha, itakuwa ni vigumu sana kwao kufikisha ujumbe kwa wazee wetu ambao wengi wao hawaelewi lugha ya kimombo. 

Huku akichangamoto, alisema ni aibu kwa wale wanaojiita wazalendo wa Kenya ilihali hawawezi kuongea lugha ya Kiswahili. Lazima tuendeleze mila zetu na tukatae katakata lugha za kikoloni. Kupitia hali hii, Wakenya watapendana na kuwa kitu kimoja. Mawazo ya Wakenya yatashirikishwa kupitia lugha yetu, na siri zetu hazitajulikana na maadui wetu. 

Katika waraka huo, Bw. Kaggiri alisema kuwa kunayo mapambano yanayoendelea kule nchini Cuba, ili kuwakomboa Wacuba ambao wamezuiliwa pale Marekani, kwa sababu ya kupigania nchi yao. Mara kwa mara kunauwezekano wa ndugu na marafiki wa Cuba kushiriki kwenye mapambano hayo. Ratiba kamili ya mpango wa kushiriki utatatolewa hivi karibu, alisema Bw. Kaggiri. 

Munala Wa Munala

Advertisements

MarchUTCbThu, 15 Mar 2007 19:45:51 +0000000000pmThu, 15 Mar 2007 19:45:51 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: