Kenya News in Swahili and English

MGAWANYIKO KWENYE CHAMA CHA ODM-K SCANDINAVIA

Kumetokea mgawanyiko mkubwa kwenya chama cha Orange Democratic Movement-Kenya Scandinavia (ODM-KS) kupitia kutangazwa kwa uchaguzi wa ugombeaji wa urais wa chama cha ODM-K nchini Kenya. 

Siasa kuhusu uchaguzi imeanza kupamba moto mjini Stockholm. Wenyeji wa mtaa huu ambao wengi wao ni wanachama wa ODM-KS, wana mtazamo tofauti kuhusu mwelekeo wa siasa nchini Kenya na hapa Skandinavia. Waandishi wa Jamii walipata fursa ya kuongea na baadhi ya wanachama na mawazo yao yalikuwa yanatofautiana sana.  

Bi. Sofia Njoroge alikuwa na maoni ya kwamba atagombea kiti cha urais kwa tiketi ya ODM-KS. Bi. Sofia alisema kwamba kutoa huduma wa kijamii kwa kutobagua watu katika misingi ya kidini, kabila, itikadi, na hata ya kisiasa, ndiyo jukwaa hasa linalotuongoza kumchagua rais wa Kenya.  

Aliendelea kusema kwamba siasa za Kenya ziko tofauti sana na sehemu zingine za ulimwengu. Watu walio nje ya Kenya wanaweza kudhani ya kwamba hali ya siasa nchini Kenya ni shwari. Mbali na hayo, aliwasihi Wakenya kumchagua yeye kama rais wa Kenya kupitia kwa chama cha ODM-KS. 

Huku tukiwa tunasubiri kwa hofu kinyang’anyiro hicho, Bi. Njoroge aliwahimiza Wakenya wanaoishi ng’ambo kuanzisha vyama vya kisiasa na kupigania uongozi kule Kenya, ili tubadilishe nchi yetu. Alisema kwamba Wakenya waendelea kuteseka kwa sababu hakuna kiongozi hata mmoja ambaye anajali masilahi ya Wakenya. Alitoa mfano wa viongozi wabaya kama vile balozi wa Kenya hapa Skandinavia, Bi. Purity Muhindi. 

Hali ya ukabila nchini Kenya imeongezeka na hata mabalozi wengi wameibeba na kuileta nchi za ng’ambo. “Tumeona watu wanakataa kumzika Mkenya mwenzao eti kwa sababu ya tofauti ya kikabila. Jee, chuki hizo zaweza kuendeleza nchi yetu kweli?” Bi. Sofia alizidi kuuliza, Kuna haja gani kwa mtu kuvaa kofia, shati na hata beji la kabila lake, wakati akijua wazi haileti picha nzuri kwa Wakenya wenzake?” 

Ushabiki kama huu unaibua na kuchochea migawanyiko kati ya Wakenya. Lazima viongozi kuchukua hatua zinazostahili kukomesha hali hii. Bi. Sofia Njoroge hana upinzani mkubwa wa karibu, kwa ugombeaji wa urais kwa chama cha ODM-KS.

Bi. Sofia aliendelea kusema ya kwamba ukweli na umakini wa utekelezaji wa ahadi zinazotolewa na wanasiasa ni miongoni mwa misingi mikuu ya demokrasia. 

Munala Munala

Advertisements

MarchUTCbTue, 13 Mar 2007 23:12:24 +0000000000pmTue, 13 Mar 2007 23:12:24 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: