Kenya News in Swahili and English

Umaskini Nchini Kenya Umeongezeka Zaidi: Ripoti Inathibitisha

Wiki mbili baada ya serikali ya Rais Kibaki kusambaza ripoti ya akaunti ya kazi yake tangu achaguliwe, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limechapisha ripoti ya kutisha, inayothibitisha kwamba umaskini umeongezeka nchini Kenya tangu 2005-2006. Baadhi ya vitu vinayochangia mateso na maisha mafupi ya Wakenya wengi ni: kukwajuka kwa hali ya afya na mazingira, ongezeko la uhalifu, na kutokujuwa kusoma na kuandika.  

Tumearidhia kwa makala mbalimbali kwenye blogu hii kwamba, umaskini nchini Kenya umezidi hata kama serikali inajivunia matokeo mema ya kazi yake. Asilimia 50 ya Wakenya wanaishi “chini ya dola moja kwa siku” na kadiri ya milioni moja hawana kazi za kufaa. Serikali nayo inajivuna jinsi ilivyoboresha maisha yao. Mikoa ya Nyanza na Magharibi inaongoza kwa umaskini na magonjwa ya kufisha, kwa sababu wengi hawana nafasi za kujipa mapato, na pia hawajui kusoma na kuandika.

Cha ajabu ni kwamba Mkoa wa Nyanza uko kwenye mpaka wa Ziwa Victoria, ambalo mapato yake kwa uvuvi wa samaki ni shilingi bilioni 41.3 ($590 milioni) kila mwaka. Isipokuwa wakaaji wa Nairobi wanaolipa kodi ya mapato ya juu zaidi nchini, Nyanza ndio inaofuatilia, na hadi makabwela wengi wanapatikana hapa. Hii ni kejeli kubwa, kwani Mkoa wa Kati unalipa robo ya ushuru ya Nyanza, na pia una tarakimu ya chini kabisa ya umaskini nchini.   

Ingawa ripoti ya UNDP imetaja hatari za aina nyingi zinazo sababisha umaskini, imemakinikia ukosefu wa usalama kwa binadamu na usimamizi mbaya wa mali ya umma. Serikali imelaumiwa kwa kutopunguza mapengo katika ugawaji wa mali/uchumi na mapato ya kibinafsi, ingawa ina sera ya kupunguza umaskini. Aina saba za hatari zimetajwa kama: uchumi, chakula, afya, mazingira, maisha ya mwenyewe, jumuia na siasa.  

Bila ushirikiano mwema kati ya serikali, taasisi mbalimbali na wananchi, hakutakuwa na maendeleo nchini Kenya. Serikali itazidi kuimba ukweli wake na kumpongeza Kibaki kwa mazuri aliyofanya, lakini tukumbuke maisha ya Wakenya wengi haijaendelezwa kamwe, tangu kubuniwa kwa serikali hii mwaka wa 2003. 

Jared Odero      (kajamii@yahoo.com)

UNDP 2006: http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=1143965449

Muluka: http://www.inequalitykenya.org/modules.php?name=News&file=article&sid=27

Ufisadi: http://www.clarionkenya.org/essay/r1_2001k.pdf

Advertisements

MarchUTCbThu, 01 Mar 2007 00:38:52 +0000000000amThu, 01 Mar 2007 00:38:52 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: