Kenya News in Swahili and English

“Tutaangamiza Ujinga Skandinavia,” Asema Bi. Hellen Opwapo

Mwenyekiti wa chama cha Orange Democratic Movement-Kenya Scandinavia (ODM-KS) Bi. Hellen Opwapo, amekaririwa akisema kuwa mojawapo ya miradi ya ODM-KS ni kuanzisha elimu ya kisiasa na historia ya Kenya hapa Sweden. Alisema haya wakati ambapo wanachama walikutana ili kupewa ripoti kutoka kwa kamati kuu ya chama hicho. ODM-KS itatoa elimu ya Siasa na Historia bure kwa Wakenya wote wanaotaka.”

Kwenye maoni yake mwenyekiti, ODM-KS inaamini kwamba wanasasia wanajukumu la kufunganisha ukuzaji wa uchumi na jamii pamoja na kuendeleza maslahi ya wasiojiweza kwanza. Aliendelea na kusema kuwa ODM-KS itaendelea kushirikiana na Wakenya kwenye mipango ya kijamii katika maeneo mbalimbali. Bi. Opwapo aliwahimiza Wakenya kuunga chama cha ODM-K mkono, kwani hicho ndicho chama cha kipekee ambacho kina mpango halisi kwa Wakenya. 

Wakati huo huo, Bi. Sofia Njoroge ambaye ni Mweka hazina wa ODM-KS, aliwashukuru Wakenya kwa kutoa fedha na kumsaidia mama mmoja mjane,  kule Korogocho mjini Nairobi, ambaye pia ameachiwa watoto wanne yatima. Aliwahimiza Wakenya kuendelea na kuwasaidia wasiojiweza kwenye jamii. Aliendelea kusema kwamba Wakenya wajitoe na kujikaza mhanga, ili tujenge nchi yetu ya Kenya. ODM-KS imejihusisha na maswala nyeti ya kisiasa na kutetea jamii ya Wakenya hapa Skandinavia na hata kwingineko. 

Kamati ya ODM-KS iliwahimiza Wakenya waendelee na kujiunga na chama cha ODM-K ili kusaidia kiutoa serikali ya Rais Kibaki, ambayo imekuwa ikiwanyanyasa wananchi wa Kenya. Bi Opwapo alinukuliwa akisema kwamba Tawi lake litaendelea na kuwa na uhusiano na jamii na kusambaza habari za ODM-K hapa Skandinavia. “Tutaendelea kutoa huduma bora kwa Wakenya, na wanakaribishwa kwenye ofisi yetu huko Högbergsgatan 48, na wawe na uhuru wa kupiga simu wakati wowote kwa sababu ODM-K ni chama cha Wakenya.” 

Hivi karibuni, ODM-KS itaanza kutoa elimu ya Sayansi ya Siasa na historia ya Kenya. Wakenya wanakaribishwa sana. Bi. Opwapo alisema kwamba elimu ni swala nyeti sana  kwa jamii, na ODM-KS itawahudumia watoto, vijana na hata watu wazima. Alisema kuwa jambo hili ni la muhimu sana kwa kuwa mradi huu utakuwa ni wa kuangamiza ujinga kati ya jamii ya Wakenya na hata Waswidi kwa jumla. 

Aliwahimiza Wakenya kuungana na kufanya kazi kwa umoja ili kujenge nchi yetu ya Kenya. Katika waraka huo, Bi Opwapo alisema kwamba ni aibu kubwa sana, kuona Ubalozi wa Kenya hapa Skandinavia umekataa kata kata kuwahudumia Wakenya. Alimuhimiza Balozi wa Kenya hapa Scandinavia Bi. Purity Muhindi, kufungua mlango kwa Wakenya kwani alitumwa hapa kuwahudumia. Hivi majuzi, Wakenya wengi wamelalamika wakisema kuwa, hakuna ufahamiano kati ya Ubalozi na Wakenya. 

Munala Wa Munala                 (kajamii@yahoo.com)

Advertisements

FebruaryUTCbMon, 26 Feb 2007 14:38:52 +0000000000pmMon, 26 Feb 2007 14:38:52 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: