Kenya News in Swahili and English

Bwana John Githongo: Shujaa au Msaliti?

Kuangamiza ufisadi ilikuwa mojawapo ya ahadi Rais Kibaki aliwapa Wakenya alipochukuwa uongozi wa nchi mwisho wa mwaka 2002. Kuthibitisha kwamba vita dhidi ya ufisadi vingepigwa, alibuni Idara ya Maongozi Bora na Maadili, akamteua Bw. John Gothongo kama Katibu wa Kudumu, mwanzoni mwa 2003. 

Bw. Githongo alipewa ruhusa na rais Kibaki kuchunguza na kuripoti kwake moja kwa moja, mambo yote yanayohusu ufisadi nchini. Fichuo kubwa kabisa katika kazi yake lilikuwa ni lile la kashfa ya rushwa ya Anglo-Leasing, iliyogharimu nchi yetu hasara ya mabilioni ya shilingi. Kashfa hii ilihusu miradi ya mazimwi yaliyobuniwa na mawaziri kadhaa na wafanyabiashara humo nchini na ng’ambo. Miradi hii haijatekelezwa hadi leo. 

Bw. Githongo alijiuzulu mwanzoni mwa mwaka wa 2005 akidai kwamba rais Kibaki, mawaziri fulani na maofisa wakuu serikalini, hawakumpa sapoti kwa kazi yake ya kufichua rushwa. Alitorokea Uingereza, na mengi yalisemwa baadaye kwamba Githongo angebaki nchini, ili kuelezea ukweli wa kashfa hii na kadhalika. Tangu aingie ukimbizini, Githongo amefichua vitu vingi na kuhojiwa kwenye njia mbalimbali za mawasiliano. Hivi majuzi, serikali ya Kenya ilidai kwamba baadhi ya wale waliotajwa na hata sauti zao kunaswa na Githongo kwenye tepurekoda, hawakufanya makosa. Kwa hivyo, “walisafishwa” ili kutolewa katika lawama ya Anglo Leasing.

Tunaposubiri uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, tukumbuke ahadi ya Rais Kibaki ya kumaliza kabisa ufisadi, na udhaifu aliyoonyesha hadi sasa. Tumkumbuke pia Bw. Githongo na majukumu aliyopewa hapo mwanzoni, kisha kuwekwa mapresha na maofisa serikalini. Ni hasara na aibu kwa nchi yetu, kwani sasa Bw. Githongo ni mkimbizi nchini Kanada, ingawa angekuwa nyumbani akifanya kazi aliyopewa na rais Kibaki. Watu fulani wanasema kwamba Githongo ni shujaa kwa kufichua kashfa ya Anglo Leasing na mengineyo, bali wengine wanamuona kama mhalifu na msaliti, kwa kuwafichua “ndugu zake”. Kwa watu hawa, rushwa ni hali ya kawaida nchini. 

   Jared Odero

  

   John Githongo: http://http://en.wikipedia.org/wiki/John_Githongo 

   Anglo Leasing: http://en.wikipedia.org/wiki/Anglo_Leasing_Scandal

Advertisements

FebruaryUTCbFri, 23 Feb 2007 13:26:52 +0000000000pmFri, 23 Feb 2007 13:26:52 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: