Kenya News in Swahili and English

Je Kuimarisha Uchumi Itaipa Serikali Ya Kibaki Kura?

Mara kwa mara Rais Kibaki na wafuasi wake wanakaririwa katika njia za mawasiliano wakisema kwamba wamefanya bidii kufufua uchumi nchini Kenya. Kwa sababu hii, wanafikiri ya kwamba wanapaswa kuridishwa serikalini baada ya uchaguzi mkuu, mwishoni mwa mwaka huu.

Ni kweli serikali hii inafanya bidii kuboresha huduma mbalimbali na kuimarisha sekta ya kilimo, inayotegemewa na Wakenya wengi. Serikali pia imefanya juhudi kuyapa majimbo yote ya uchaguzi, mamilioni ya fedha, ili miradi tofauti ianzishwe. Hii ni sawa, isipokuwa kuimarisha uchumi isiwe tu ndio mahubiri ya kutafuta kura kwa wananchi.  

Hapa Sweden, matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yalistaajabisha serikali ya wakati huo (Social Democratic Party) iliyotawala miaka 12, na hata kuimarisha uchumi. Swala ambalo liliwaangusha lilikuwa ni la kuwapa watu kazi, ila hawakulishugulikia, wakidhani kwamba Waswidi walifurahia uchumi uliyo imara. Wapinzani wao nao walizunguka zunguka nchini wakihubiri na kuahidi kazi, kama wangepigiwa kura.

Cha ajabu ni kwamba waaumini wengi wa serikali hiyo ya zamani waliwapa kura zao muungano wa upinzani, ambao sasa unatawala. Wengi walikuwa wameshachoka na maneno ya waziri mkuu wa zamani, kwani alianza kuwa na kiburi. Alikuwa na hakika wangepata kura na kurudi serikalini, kulingana na rekodi yao nzuri ya uchumi. 

Tukirudi nchini Kenya, twaona kwamba rais Kibaki anaonyesha mtindo huo huo wa kiburi na maringo. Nampongeza kwa juhudi zake, isipokuwa kuna wakati maneno yake ni yale ya mtu aliyeanza kujisifu kabla hata ya kumaliza mbiyo. Rais huwa anawakemea wapinzani wake kwa kuwaita “Pumbavu, Mavi ya Kuku, Bure Kabisa” na kadhalika. Huu ni ujeuri mkubwa, kwani kiongozi anapaswa kuepuka matusi, hata kama anashutumu. Isitoshe, waziri wa Sheria Bi. Martha Karua, huwa hafichi ujeuri na ukaidi wake, anapowakemea wapinzani wa serikali. 

Ukosefu wa kazi nchini Kenya ni hofu kubwa kwa wananchi wengi. Licha ya hayo, kuna ushahidi kwamba watu fulani wanaajiriwa kulingana na makabila yao, mapendeleo au uhusiano wao kisiasa. Hii inazidisha pengo katika mapato ya kibinafsi. Uwongo mkubwa wa serikali ya Kibaki katika kampeni za 2002, ni ahadi ya kubuni kazi kwa watu laki tano kila mwaka. Ingawa vijana wengi wanakamilisha masomo kila mwaka, wengi wao hawapati kazi kamwe.  

Mwaka jana waziri wa ujenzi wa barabara Bwana Nyachae, alizipa sehemu zinazo sapoti serikali pesa nyingi za kutunza mabarabara, zaidi ya sehemu za upinzani. Hii ni kinyume cha ahadi ya rais Kibaki kuwatumikia wote bila ubaguzi. Ikiwa bajeti ya miradi ya maendeleo itaendelea kugawanywa kwa hali hii, basi inathibitisha hofu ya wengi kwamba serikali haina haja ya kusawazisha utajiri ili kuangamiza umaskini. 

Serikali ya rais Kibaki inapaswa kufikiria na kurekebisha hali mbaya ya usalama inayotisha wananchi kutokana na ongezeko la ujambazi, ili kuwapa amani. Hata kama wito wa rais ni “taifa la kazi”, anakumbushwa kwamba raia wengi wako mbali na hali hii, na watafikiria njaa, umaskini na mateso waliyopitia kwa miaka mitano, watakapo piga kura. 

Jared Odero (Tuma maoni kwa: kajamii@yahoo.com)

Advertisements

FebruaryUTCbSun, 18 Feb 2007 00:15:55 +0000000000amSun, 18 Feb 2007 00:15:55 +000007 19, 2007 - Posted by | Siasa

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: