Kenya News in Swahili and English

“MAPAMBANO YATAENDELEA” ASEMA MARTIN NGATIA

Naibu wa Mwenyekiti wa chama cha Orange Democratic Movement-Kenya Scandinavia (ODM-KS) Bw. Martin Ngatia, amekaririwa akisema kuwa Serikali ya Kenya lazima ifuate maadili walioandikiana na Wakenya.  

Kwa maoni yake, ni kinyume cha sheria kulingana na umaskini nchini, kuwalipa wanabunge mishahara mikubwa, hali wanaandaa vikao chache kabisa bungeni kila mwaka. “Wakenya wanaendelea kulipa watu ambao hawafanyi kazi. Huu ni wizi wa hali ya juu kabisa, na lazima tukatae katakata serikali kama hii ambayo inaendelea kuwanyanyasa wananchi kwa kuwaibia pesa zao za ushuru”. Bw. Ngatia alinukuliwa akisema haya wakati ambapo chama chake cha ODM-KS kinapanga jopo ambalo litasaidiana na matawi mengine ya ng’ambo ili waone ODM-K imeshinda kwenye uchaguzi wa mwaka huu. 

Serikali inatakiwa pia kuhakikisha kuwa vyama vya siasa vya upinzani vipewe ruzuku ili viwe na utaratibu wa sawa na chama kinachotawala. Katika hali hii, tutakuwa na ushindani ulio sawa wakati wa uchaguzi. Awali, Bw. Ngatia alisema kuwa ODM-K itashinda kwenye uchaguzi ujao iwapo watabaki kuwa kitu kimoja. Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu”, alisema Bw. Ngatia. ODM-K lazima iendelee na kuunganisha vyama vya kisiasa vyenye usajili wa kudumu, ili viweze kuleta upinzani mkuu kwenye uchaguzi wa mwaka huu. 

Ngatia aliendelea na kuikosoa Serikali ya Kibaki akisema kuwa Kibaki alienda kinyume cha maadili aliyosaini kabla ya uchaguzi wa 2002, na akawahimiza Wakenya wawe macho wakati huu, ili wasidanganywe tena. Aliwasihi pia viongozi wa ODM-K waheshimu maadili watakaosaini kati yao. “Nchi yetu bado changa sana kwa demokrasia ya vyama vingi, licha ya kuwa na vyama vingi”, Bw. Ngatia alikaririwa. Alizidi kawahimiza viongozi wa ODM-K kuonyesha vyama vingine njia nzuri ya demokrasia, ili kuleta msisimko wa Siasa nchini Kenya. 

Vilevile, katika waraka huo wa marekebisho, aliwaomba viongozi wa ODM-K kuunguna kwa lengo moja la kumtoa Raisi Kibaki, la sivyo itakuwa vigumu sana. Bw. Ngatia aliwatakia kila la heri kwenye maandamano ya leo (17/02/07) na akawahakikishia Wakenya kuwa Mapambano bado Yataendelea! 

Munala wa Munala (Tuma maoni kwa: kajamii@yahoo.com)

 

Advertisements

FebruaryUTCbSat, 17 Feb 2007 15:07:36 +0000000000pmSat, 17 Feb 2007 15:07:36 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: