Kenya News in Swahili and English

Shukrani Kwa Kenya Stockholm Blog (KSB)

Kwa niaba ya waandishi wote wa Jamii, tungependa kuchukua fursa hii kurudisha shukrani zetu kwa KSB. Salamu zetu zimwendee Bwana Okoth Osewe na waandishi wote wa KSB, kwa kututambua na kushirikiana nasi katika blogu yao.                             

KSB ni mtambo mmoja wa sifa, sio hapa tu Sweden, bali hata kwingineko ulimwenguni. Waandishi wake wana ushupavu na akili za kufichua siri na kutatua matatizo zinazohusu Wakenya, kwa kufuata viongo na vidokezi wanavyovigundua kupitia kwa njia za ushirikiano na Wakenya.

Habari za Jamii zimeanza kuvuma kwa mlio mmoja. Ni matumaini yetu kwamba tutaendelea kutunza mradi huu na tutashirikiana na KSB na wengineo, kwa kuelimisha, kukosoa, kurekebisha na kukaribisha mijadala ya aina nyingi. Hatua za mwisho zimekamilishwa katika juhudi za kuwakaribisha watakaochangia habari kwa mradi huu wa Jamii.

Tunaendelea kuunda jopo la wataalam na washauri kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, na KSB ni mojawapo. Kazi ya jopo itakuwa ni kusoma, kuchanganua na kuhariri habari za jamii. Kupitia hali hii, tutajadili maneno, fasili maana na matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili, na hata kuwajibu wasomaji wetu barua nyingi ambazo zimetufikia hadi leo.

Sifa mojawapo ya Jamii ni kwamba inakusanya na kushirikisha mawazo ya Wakenya kwa jumla. Ni matumaini yetu ya kwamba tutashirikiana katika kuimarisha mradi huu. Kwa niaba ya waandishi wote wa Jamii, tunawashukuru wasomaji wetu wote. Asanteni!

Munala wa Munala na Jared Odero

Advertisements

FebruaryUTCbFri, 16 Feb 2007 14:16:34 +0000000000pmFri, 16 Feb 2007 14:16:34 +000007 19, 2007 - Posted by | Salamu, Barua na Vichekesho

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: