Kenya News in Swahili and English

Je Twarejea Gizani Kisiasa Nchini Kenya?

Ni sikitiko kubwa sana kwamba demokrasia nchini Kenya iko katika hali ya tisho na hatari kubwa, kutokana na kupigwa marufuku maandamano ya kupinga siasa mbaya. Akitoa amri hii kwa niaba ya serikali, Waziri wa usalama wa ndani Bw. John Michuki, juzi alisema kwamba hamna atakaekubaliwa kuandamana bila ruhusa maalumu, kutoka kwa kamati mbali mbali za usalama wilayani.        

Katika nchi za kidemokrasia, maandamano yanafanywa kuonyesha kuchukizwa au kutoridhika na vitu fulani. Baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini Kenya wameshutumu amri hii, na kuonya serikali ya Rais Kibaki kwamba imeanza udikteta na ikiendelea, basi wananchi watajitokeza kwa wingi kuandamana. Hivi majuzi, Bwana Michuki aliwaonya wafanyakazi wa utawala (wakuu wa mikoa na wilaya, machifu na kadhalika) kwamba lazima wawe watiifu na waaminifu kwa serikali, kwani wameongezewa mishahara. Hii inafasiriwa kwamba wamehongwa ili wanyamaze na kufuata amri bila maswali.

Wengi wetu twakumbuka siasa mbaya za miaka ya 1980 hadi 1992, tulipopigania na kushinda haki za kuwa na serikali yenye vyama vingi. Ni kejeli kwamba hawa wanaotawala sasa hivi, ndio waliopigania haki hizo wanazotukataza. Wenzanguni, Katiba ya nchi imetupa haki za kutoa maoni yetu na kushirikiana, bora tusivunje sheria. Popote tulipo, tusikubali kamwe serikali ya Kibaki kuturejesha gizani kisiasa.

Tuitunze demokrasia yetu iliyo changa, ili tuboreshe maisha yetu na wale watakaokuja baadaye. Tusikubali kunyang’anywa mapato mema ya demokrasia hii, kwani yataleta athari hasi kwa maaendeleo.

Jared Odero na Munala wa Munala 

Advertisements

FebruaryUTCbThu, 15 Feb 2007 12:00:26 +0000000000pmThu, 15 Feb 2007 12:00:26 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: