Kenya News in Swahili and English

MUNGIKI AU SERIKALI YA MASKINI?

Kuna wasiwasi unaoonekana kutanda katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya, kuhusu kuendelea kwa shughuli za magenge ya wahuni katika maeneo ya makazi duni, jambo ambalo linaoonekana kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa sheria katika jamii hizo. Mungiki ni moja ya magenge hayo ya wahuni. Kikundi hicho kinasadikika kueneza kurejewa kwa imani za jadi za kabila la kikuyu; lakini hata hivyo kimetuhumiwa kwa mauaji, unyang’anyaji na ulaghai.  

Wafuasi wa kikundi hicho wanafanya shughuli zao katika maeneo ya Mathare, Kibera, Korogocho na vitongoji vya makazi duni. Kila nyumba inalipa kati ya shilingi 200-1000 kila mwezi kwa ajili ya usalama, na shilingi 200 kwa mwezi kwa ajili ya umeme. Genge hilo limechukua kazi ya ujenzi wa vyoo vya umma, na kudai kila mtu alipe ada ya matumizi ya choo kama shilingi 200 kwa mwezi, kiwango ambacho wengi hawawezi kulipa kutokana na umasikini walio nao. Hali hii imesababisha msuguano kati ya magenge na watu masikini.

Mwaka jana, genge hilo lilianza kudhibiti biashara yenye faida ya “chang’aa” (pombe) kwa madai kwamba watengenezaji walitakiwa kulipa ada ya shillingi 2000. Watengenezaji walipinga madai hayo na hapo genge hilo liliharibu biashara hiyo. Katika jitihada ya kutuliza hali, ufumbuzi wa matatizo ulitokea. Wengi waliohusishwa kwa matatizo hayo walidai kwamba kama serikali ingetimiza wajibu wake kwa kujenga makazi na huduma zingine za msingi kama maji na umeme, basi hawangetaabishwa na genge hilo. Umasikini umewalazimisha wakaaji wa vitongoji hivyo kufanya biashara ambazo serikali inadai siyo halali. Mwaka 2003, serikali ilitangaza kwamba ingejenga nyumba zaidi ya 150,000 kwa watu wa makazi duni. Miaka mitano baadaye, ahadi hii bado haijatekelezwa. Wakenya wenzangu, inapaswa kubadili mfumo mzima wa utawala, na jambo muhimu zaidi ni kuwa na sera ya kutoa mwongozo wa makazi na kutoa huduma katika maeneo ya makaazi duni.

Serikali ya Kibaki imeshindwa kuwasaidia wakaaji hawa katika kipindi hiki. Wakazi hawa wamechanganyikiwa akili na kushindwa kwa nini serikali haiwezi kuwapatia makazi au huduma. Wakaaji wa Kibera, Mathare na Korogocho yafaa wajitoe na uzoefu wao, hofu zao na matarajio na kuonyesha dunia vile wanavyokabiliana na hali kama hii isiokuwa ya kibinadamu. Mara nyingi watu ambao hawaishi katika makazi duni ndio ambao wanazungumzia masuala kuhusu makazi duni. Wakati huu, serikali ya Kibaki imewaangusha tena. Asilimia 60 ya wakaaji wote wa mji mkuu wa Kenya wanaishi katika makazi duni na hawawezi kuishi maisha ya heshima. Serikali imeshindwa! Kibaki asipewe kipindi kingine mbali Wakenya wamchague rais tofauti kuona kama watapata mabadiliko, kwani masilahi ya binadamu ni ya maana kuliko vitu vingine.

Hivi leo, bwana Michuki (waziri wa usalama wa ndani)  na jeshi lake wamemeua sheria moja ya demokrasia. Bwana Michuki ni mwongo na mwoga ambaye anaogopa maendeleo ya wananchi wa kawaida. Majuma mawili yaliyopita kwenya Kongomano la Kijamii Duniani (World Social Forum), vijana kutoka makaazi duni waliandamana wakisema ya kwamba Michuki amewaibia masikini. Hii imedhihirishwa wazi leo kuwa bwana Michuki ni mnyonyaji haramu ambaye hajali masilahi ya Mkenya wa kawaida.

Bwana Michuki, heshimu demokrasia na Wakenya waliokuchagua kuwaongoza. Kenya sio biashara yako ya kibinafsi ambayo utafungia watu kuandamana kwa maovu unayotenda. Wakenya wamekomaa kisiasa na hawatakubali kurudishwa nyuma na ukoloni mamboleo.


Munala Wa Munala

Advertisements

FebruaryUTCbTue, 13 Feb 2007 23:07:34 +0000000000pmTue, 13 Feb 2007 23:07:34 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: