Kenya News in Swahili and English

Ufisadi Unazidisha Umaskini Nchini Kenya

Wakenya wenzangu, tuchukue jukumu na tufanye bidii kuendeleza maslahi ya jamii, kwani ndio msingi bora wa kugawanya mali nchini. Kinyume chake ni maslahi binafsi, inaowatajirisha wachache kati ya maskini walio wengi. Kugawanya mali kwa usawa itawapa maskini fursa ya kushirikiana katika kujenga taifa, ili sote tuweze kuwa na maisha bora.  

Kwa sasa, kuna pengo kubwa kati ya mamilioni ya wananchi walio maskini, na wale wachache walio matajiri. Kenya imebarikiwa na mali asili, lakini hatuna usawa katika kugawanya rasilmali tunapofaidika. Sipingi kwamba kuna wale waliopata mali kwa kufanya bidii, ila nasikitika kwamba wengi hawana nafasi hata ya mapato kidogo ya kusaidia familia na jamii zao. Nikitumia mfano wa Sweden, nchi iliyoendelea, historia inaonyesha kwamba kwa miaka mingi, serikali zilizoitawala zimekuwa zikitia maanani ugawanyaji na usawazishaji wa mali, ili kuendeleza maslahi ya jamii. Matokeo ni kwamba wananchi wanapata masomo ya bure kuanzia shule za watoto wadogo (chekechea), hadi vyuo vikuu. Ingawa Waswidi wanatozwa ushuru na kodi za juu, serikali inahakikisha kwamba wanapata huduma bora na hali njema ya maisha kwa kuwajengea mashule, mahospitali, mabarabara na kadhalika.

Mswidi hana wasiwasi kwamba hatapata kitanda hospitalini, ama kukanwa matibabu kwa ajili ya kukosa pesa zakulipa. Wote wanahaki ya kupata matibabu bora katika hospitali yoyote nchini wakiwa wagonjwa. Hivi sivyo ilivyo nchini Kenya, ambapo kama wewe ni fukara, basi sahau matibabu bora, kwani hospitali nzuri zimeteuliwa kuwahudumia matajiri. Ingawa Wakenya wengi wanalipa ushuru na kodi nyingi, huduma bora zimekosa katika sekta na idara mbali mbali. 

Ndugu Munala wa Munala amenena vema kwamba lazima tushutumu ufisadi na uongozi unaoendeleza ukabila nchini Kenya. Maendeleo ya Wakenya inawezekana tu kama kuna uongozi bora unaotuwezesha kugawanya na kutumia utajiri kwa usawa. Umaskini unazidi nchini, hali kuna wachache ambao utajiri wao unashangaza, hata ukilinganisha na ule wa nchi zilizoendelea. Matokeo ya uchunguzi tofauti yanaonyesha kwamba matajiri wengi nchini Kenya wamepata mali zao kutokana na ufisadi. Kuna uhusiano mkubwa kati ya ufisadi na umaskini, kwani ufisadi ni wizi wa mali ya umma. Nawasihi tushirikiane ili tumilikwe na viongozi watakaoshugulikia mahitaji yetu.  

Jared Odero 

 

Advertisements

FebruaryUTCbMon, 12 Feb 2007 15:44:24 +0000000000pmMon, 12 Feb 2007 15:44:24 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: