Kenya News in Swahili and English

Wazo La Siku

Sasa ndugu na dada zetu, asili ya maisha yetu haya tulio nao ni ipi? Hebu tuipeleleze! Maisha yetu ni ya taabu, yenye kuchosha, na mafupi. Katika dunia yetu hakuna Mkenya mwenye uhuru. Maisha ya Wakenya imekuwa ni ya shida na ya utumwa. 

Je, hii ni sheria ya maumbile yetu? Je, ni kwa kuwa Kenya ni nchi maskini isioweza kutoa maisha bora kwa wote waishio juu yake? Udongo wa nchi yetu ni wenye rutuba, na waweza kutoa chakula kingi kwa Wakenya wote. Kwa nini basi tunaendelea kudhulumiwa? Ni kwa sababu mazao yetu yote yanaibiwa na wakoloni mamboleo na mabepari.

Tukiwaondoa hao wakoloni mamboleo kabisa, shida zetu zitapungua sana. Hawa wakolono mamboleo na mabepari ni wanyonyaji haramu, na hawafikirii lolote kuhusu maisha yetu ya taabu. Sisi hatunung’uniki, maana ni ukweli mtupu. Kwa hiyo Wakenya wenzetu, ni wazi kwamba ubaya wa maisha yetu haya watokana na udhalimu wa viongozi wabaya. Tukiepukana na viongozi hawa tutaona mabadiliko makuu nchini Kenya. Siku fulani tutakuwa wenye mali na walio huru. Mwaka huu tutawachagua viongozi watakao tuongoza kwa miaka mitano zijazo.

Je, tutakubali koungozwa na Mawaziri/Wanabunge waliohusishwa na ufisadi kama vile Michuki, Saitoti, Murungaru, Kiraitu na wengineo? Tuwachague viongozi watakao tutumikia, sio tu kwa maneno matamu ya kutoa nyoka pangoni, lakini utumishi kwa matendo na maslahi ya Wakenya wote.

Odero Jared na Munala wa Munala 

Advertisements

FebruaryUTCbMon, 12 Feb 2007 19:38:48 +0000000000pmMon, 12 Feb 2007 19:38:48 +000007 19, 2007 - Posted by | Uncategorized

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: